Kama tunavyojua ujauzito unapo haribika tumboni basi litachukuliwa jukumu la kusafisha na kuacha tumbo likiwa salama, lakini hii imekuwa tofauti kwa mwanamama mmoja kutoka China aliyetambulika kwa jina la Huang Yijun, ambaye aliendelea kubeba mtoto wake aliyekufa tumboni kwa miaka 60.
Mwaka 1948 akiwa na umri wa miaka 31 alipata ujauzito ambao kwa mujibu wa madaktari haukuwa wa kawada (ulikuwa wa nadra) kwani aligundulika kuwa na tatizo la ‘Ectopic Pregnancy.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya walimpatia ushauri mwanamke huyo aweze kutoa mtoto kijusi hicho kwani ujauzito huo ulikuwa na asilimia moja ya kuisha na endapo mtoto huyo angezaliwa angekuwa na asilimia 21 ya kuwa mlemavu.
Kwa bahati mbaya, wakati huo gharama ya upasuaji wa kumtoa mtoto zilikuwa kubwa, jambo ambalo lilimfanya mwanamke huyo kushindwa gharama na kuacha mtoto huyo aliyekufa kubaki tumboni mwake.
“Ilikuwa kiasi kikubwa sana wakati huo, zaidi ya kile familia yangu ingeweza kupata kwa miaka kadhaa, kwa hivyo sikufanya chochote na nikalipuuza,” Huang alisema katika moja ya mahojiano yake.
Baada ya miaka 60, mtoto aliyekufa tumboni alibadilika na kugeuka kuwa mgumu kama jiwe. Hii hutokea kwa sababu madini ya kalsiamu hujikusanya kuzunguka tishu zilizokufa, na kumfanya kijusi hicho kuwa 'mtoto wa jiwe,' au kwa kitaalamu, 'lithopedion'.
Huang aliendelea kuishi na mtoto wa jiwe tumboni mwake mpaka alipofikia umri wa miaka 92 mwaka 2009 ndipo alifanyiwa upasuaji na kuondoa kijusi hicho kilichoonekana kuwa kimekauka na kuwa na asili kama jiwe.
Chanzo News 18.

Leave a Reply