Mfahamu mwanamke aliyebana kiuno, tumbo ili kumridhishe mumewe

Mfahamu mwanamke aliyebana kiuno, tumbo ili kumridhishe mumewe

Aliyesema mapenzi upofu wala hakukosea, kwani watu hujikuta wakifanya baadhi ya mambo kwa lengo la kuwaridhisha wanaowapenda. Kutokana na mapenzi mfahamu Ethel Granger mwanamama ambaye alipitia maumivu makali kwa ajili ya kumridhisha na kumfurahisha mumewe.

Ethel raia wa Uingereza akiwa na miaka 23 alianza kuvaa nguo aina ya korseti inayobana tumbo na kiuno ili kupunguza ukubwa wa kiuno kwa ajili ya kumfurahisha mume wake William Arnold Granger.

Baada ya wawili hao kufunga ndoa mwaka 1928 mume wa Ethel alikuwa akivutiwa zaidi na wanawake wenye viuno vyembamba hivyo aliamua kumshawishi mke wake kuvaa nguo za korseti ili kubana kiuno chake kiweze kuwa chembamba.

Licha ya mwanamke huyo kupata maumivu mwanzoni wakati wa kuvaa vazi hilo lakini mumewe aliendelea kumshawishi avae hivyo mpaka wakati wa kulala.

Kwa kuwa William alikuwa ni mtu wa kufuatilia sana mitindo alimtaka mwanamke wake kuvaa hereni maalumu aliyomtengenezea iliyopanua sikio lake hadi kufikia 8mm pamoja na kutaka avae viatu virefu wakati wote anapokuwa nyumbani.

Baada ya miaka kadhaa, mwanamama huyo aliingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunaia 'The Guinness Book of Records’ kwa kuwa mwanamke mwenye kiuno kidogo zaidi kiuno chake kikiwa na inchi 13 (sentimita 33).

Ikumbukwe kuwa Ethel Granger alizaliwa Aprili 12, 1905 na alifariki dunia Januari 1982 huku mume wake William Arnold Granger alizaliwa 1903 na alifariki Machi 1974

Chanzo tovuti ya (Glamorous Corset).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags