Mfahamu mbunifu wa bendera ya Marekani

Mfahamu mbunifu wa bendera ya Marekani

Msemo wa 'Mwalimu wa mathe hapa ni wapi?', unaendana na stori ya Robert Heft, ambaye mwaka 1958 akiwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17, alibuni bendera ya Marekani yenye nyota 50.

Ubunifu wa Robert ulitokana na kazi ambayo walikuwa wamepewa na mwalimu darasani, ambapo katika matokeo ya ubunifu huo mwalimu alimpatiwa alama B, ambayo Robert hakuifurahia, kwani aliamini amefanya kazi nzuri iliyopaswa kuwekewa A+.

Hata hivyo, aliyekuwa Rais wa Marekani kipindi hicho Dwight Eisenhower, alikuwa ameagiza kupelekewa bendera mbalimbali ili achague itayofaa kutumiwa kwenye taifa hilo baada ya jimbo jipya kujiunga na Marekani.

Kabla bendera ya Robert haijapelekwa kwa Rais, alimhakikishia mwalimu kuwa itachaguliwa na mwalimu ataona aibu kwa kuwa alimpatia alama B.

Baada ya bendera kupelekwa kwa Rais ya Robert ilichaguliwa kati ya 1500, zilizokuwa zimepelekwa, kitendo hicho kilimfanya mwalimu abadili alama za mwanzo na kumuwekea A+.

Ubunifu wake haukuishia hapo mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 67, kabla ya kifo chake alikuwa tayari amebuni bendera nyingine yenye nyota 51 ambayo ingetumika kama jimbo jingine litaongezeka. Robert alizaliwa mwaka 1941, alifariki dunia 2009.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags