Mfahamu binti mwenye aleji na maji, Akioga hutokwa damu

Mfahamu binti mwenye aleji na maji, Akioga hutokwa damu

Inafahamika kuwa maji muhimu katika maisha ya kiumbe hai, kwa mimea yanahitajika kwa kiasi kikubwa, wanyama na hata binadamu pia kwani hutumia kama kinywaji na katika matumizi mengine.

Lakini uwepo wa maji duniani umekuwa ukimpatia mateso makubwa msichana Tessa Hansen-Smith, mzaliwa wa Fresno, California, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ana ‘aleji’ na maji na endapo akitumia au kumgusa hupata matatizo makubwa hadi kutokwa damu kichwani.

Tessa, alizaliwa akiwa na afya njema ambapo alikuwa na uwezo wa kutumia maji, alioga, kunywa na hata kufanyia matumizi mengine lakini alipofika umri wa miaka 8 mambo yalibadilika badala yake maji yakageuka na kuwa mateso kwake.

Binti huyo hupata maumivu makali endapo mwili wake utaguswa na maji, hutoka vidonda , vipele, kuwashwa na kutokwa na damu kwenye ngozi ya kichwa endapo ataosha nywele zake au kuoga.

Na imeenda mbali zaidi kwani msichana si maumivu tu akitumia maji bali hata vimiminika vitokavyo mwilini kama vile ,jasho, machozi na mate bado humpatia maumivu vikimgusa.

Anaeleza kuwa kabla ya kufahamu tatizo lake ilikuwa ni jambo la kutisha kwa familia yake kwani kila alipooga alitoka vipele, ngozi kuvimba na hata kutoka damu kichwani.

lipelekea wazazi wake watupe sabuni zote za kuogea wakidhani ndiyo tatizo kwake, lakini haikuwa hivyo vipimo vya daktari viliweka wazi kuwa binti huyo ana ‘aleji’ ya maji ambayo kitaalam inaitwa Aquagenic Urticaria ( Water Allergy).

Akinywa maji hujikuta akihisi maumivu makali ya kuungia kwenye koo lake kutokana na hilo hulazimika kutumia maziwa kukata kiu, kwani yana kiwango kidogo zaidi ni protini, mafuta na sukari.

Kwa ajili ya kusafisha mwili wake ili kuondokana na harufu amekuwa akitumia ‘taulo’ maalumu zenye unyevu kwa ajili ya kujifuta lakini bado pia humletea maumivu makali.

Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya, Fresno, California, hali hiyo huitwa Aquagenic Urticaria, na inaelezewa kuwa  imewapata takribani watu 250 duniani kote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags