META kuzindua miwani itayofanya shughuli za kwenye simu

META kuzindua miwani itayofanya shughuli za kwenye simu

Kampuni ya Meta ipo mbioni kuja na miwani mpya yenye teknolojia ya hali ya juu ambayo inatajwa kuwa na uwezo wa kuunganisha ulimwengu wa kidigitali.

Miwani hiyo iliyopewa jina la Orion inatajwa itakuwa na uwezo wa kuonyesha taarifa moja kwa moja kwenye lenzi za miwani, kama vile ujumbe wa sms za simu, na taarifa nyingine, bila hitaji la kutumia simu ya mkononi moja kwa moja.

Miwani hiyo inalenga kuleta mapinduzi kwenye sekta ya teknolojia ya kuvaa (wearables) kwa kutumia teknolojia za ukweli uliodhabitiwa (augmented reality - AR) na kuifanya iwe rahisi kwa watumiaji kuingiliana na mazingira yao kwa kutumia taarifa za kidigitali zinazojitokeza katika wakati halisi.

Aidha, miwani hiyo itakuwa na vitu kama vile kamera, spika, na viunganishi vya kidigitali, ingawa bado haijatolewa rasmi licha ya Mtendaji Mkuu wa, Mark Zuckerberg alisema anatarajia miwani hiyo kubadili ulimwengu.

Katika maoni yake, Zuckerberg alieleza kuwa anatarajia miwani hiyo itabadili jinsi watu wanavyoingiliana na teknolojia ya kidijitali na ulimwengu halisi. Alisisitiza kuwa teknolojia kama hii ni sehemu ya lengo lake la kuendeleza "metaverse" ulimwengu wa mtandaoni ambapo watu wanaweza kufanya kazi, kucheza, na kuwasiliana kupitia vifaa vya hali ya juu kama miwani ya Orion.

Pamoja na hayo, amesema miwani hii itaongeza urahisi na kuweka teknolojia karibu zaidi na maisha ya kila siku bila kuhitaji vifaa vikubwa kama simu au kompyuta za mkononi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post