Messi na Ronaldo kukutana Februari 1

Messi na Ronaldo kukutana Februari 1

Baada ya kuzuka tetesi kuhusiana na ‘klabu’ ya Inter Miami kuingia dimbani na ‘timu’ ya Al Nassr, sasa uvumi huo umethibitishwa kuwa ukweli, ambapo miamba wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Mess wanao kipiga katika ‘vilabu’ hivyo viwili watakutana tena Februari 1 mwaka 2024.

Aidha kupitia ukurasa wa Instagram wa Inter Miami wameshusha mkeka mwingine kupitia ‘klabu’ hiyo hiyo anayo ichezea Messi itakipiga tena Januari 29 na ‘klabu’ ya Al Hilal anayoichezea Neymar ikiwa ni michezo ya kirafiki ya kujiandaa na kuendelea kwa msimu.

‘Mechi’ zote mbili zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kingdom Arena uliyopo mji mkuu wa Saudi Arabia.

Ikumbukwe kuwa mchezo wao wa mwisho ulikuwa Januari mwaka huu ambapo Messi aliingia dimbani akiwa na ‘klabu’ yake ya zamani ya Paris Saint-Germain na kuipatia ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Riyadh all-star XI iliyohusisha wachezaji wa Al-Hilal na Al Nassr anayoichezea Ronaldo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags