Meli kubwa zaidi duniani kuanza safari mwezi ujao

Meli kubwa zaidi duniani kuanza safari mwezi ujao

Meli kubwa zaidi duniani ya kitalii iitwayo "Icon of the Seas" inatarajia kuanza safari Januari 27, 2024, kutoka PortMiami nchini Marekani, na itaanza kwa ziara ya siku saba ya  Caribbean.

Katika safari zake "Icon of the Seas" inatarajiwa kubebea abiria 7,600 na wafanyakazi 2,350, meli hii ina urefu wa mita 365 na uzani wa tani 250,800 na itakuwa kubwa zaidi kuipita "Wonder of the Seas," kwa ukubwa na uwezo.

"Icon of the Seas", inasehemu kwa ajili ya familia, bustani, sehemu ya kuogelea, club na sehemu nyingine nyingi za kula bata. meli hii imetengenezwa na Royal Caribbean International, matengenezo yake yalianza mwaka 2016 na hadi kufikia mwakani itaanza kazi za usafirishaji.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags