Mejakunta: Hakuna msanii wa singeli anayenifikia

Mejakunta: Hakuna msanii wa singeli anayenifikia

Msanii wa Singeli hapa nchini, Mejakunta ametamba na kusema kuwa kwa sasa hakuna msanii wa miondoko hiyo ya Singeli anayemfikia kwa namba katika mtandao wa YouTube.

Mejakunta ametamba kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii nchini Tanzania ambaye nyimbo zake za singeli zinaongoza kwa kuangaliwa kwa wingi katika mtandao wa YouTube.

“Muziki unatembea kwa namba, hata wakina Diamond wanawekaga namna ambavyo wanaongoza kwa namba huko mitandaoni, muziki ili uheshimike lazima uwe na namba kwani ni kitu muhimu,

“Ukiibeza kazi yangu sijui imefanyaje mimi nakuona kama shabiki tu ambao wanaongea tu ila nikwambie hakuna msanii yeyote wa singeli anayeongoza tofauti na mimi,” amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags