Megan: Siwezi kuwa chumba kimoja na Tory

Megan: Siwezi kuwa chumba kimoja na Tory

Rapa kutoka nchini Marekani Megan Thee Stallion bado anasumbuliwa na tukio la kupigwa risasi na Tory Lanez anasema hawezi kuwa katika chumba kimoja na Tory ambaye ndiye alimfanyia kitendo hicho.

Kwa mujibu wa TMZ news inaeleza kuwa ‘rapa’ huyo hakuwepo mahakamani siku ya jana kwa ajili ya hukumu ya Tory.

Mwanadada huyo anaeleza kuwa bado hajawa na amani tangu apigwe risasi Julai 2020 na Tory.

Tory alitarajiwa kuhukumiwa siku ya jana, lakini ‘kesi’ ilisogezwa mbele hadi siku ya leo Jumanne. Huku waendesha mashtaka wanataka hakimu amhukumu Tory kwa angalau miaka 13 jela, ingawa anatafuta kifungo kifupi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags