Meek Mill: Wafungwa wanafanya kazi nyingi lakini wanalipwa kidogo

Meek Mill: Wafungwa wanafanya kazi nyingi lakini wanalipwa kidogo

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani #MeekMill amefunguka kuwa kazi za wafungwa wakiwa gerezani huwa ni nyingi sana kuliko malipo wanayopata nchini humo.

‘Rapa’ huyo ametoa maoni yake kuwa unaweza ukawa tajiri na unapesa za kutosha lakini ukiwa mfungwa unaamshwa saa 11 alfajiri kufanya kazi kwa malipo ya senti 12 kwa saa.

#MeekMill aliwahi kuhukumiwa jela mwaka 2016 na alitoka mwaka 2018 kwa makosa ya madawa ya kulevya na umiliki wa silaha kinyume na sharia. Ikumbukwe kuwa wafungwa katika baadhi ya mataifa ulipwa pesa kutokana na kazi wanazofanyishwa wakiwa gerezani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags