Mchongo wa Kontawa kwenda jeshini uko hivi.., atuma dedication kwa Zee Cuty

Mchongo wa Kontawa kwenda jeshini uko hivi.., atuma dedication kwa Zee Cuty

Kama ilivyo kawaida yetu ni mwendo wa ma-exclusive tu hahaha hatutaki utani sisi, na wala hatupendi mwanafamilia wetu wa Mwananchi Scoop ukae na maswali meengiii kuhusu watu maarufu kwenye tasnia mbalimbali.

Ukisiki mwanangu ‘Dunga Mawe’, ‘Mi Nachekaga Tu’ ‘Mwalimu’ na mzee wa ‘Champion’ nadhani utakuwa umeelewa ni nani anazungumziwa na bila kupoteza muda leo tuko na mwanetu Kontawa akitusanua mengi kumuhusu.

Kwanza kabia bila ya kuchelewa mkali yupo ana jiwe lake jipya mjini linaitwa ‘Wewe’ na kizuri zaidi mzigo huko mjini YouTube umetembelewa na wageni kibao yaani namba zinasomeka haswaaaaaa.



Mwananchi Scoop kama kawaida ikaona siyo mbaya kama itapiga story mbili tatu na Tawa mwenyewe, wengine siku hizi wanamuita ‘Mwalimu’, kwa heshima kubwa nikwambie kuwa wimbo wake mpya wa ‘Wewe’ hadi sasa unaendelea kufanya vizuri.


Kutokana na ngoma za mkali Kontawa mara nyingi hukubaliwa na mashabiki wa kila rika Mwananchi Scoop tukaona si mbaya kama tukifahamu idea nzima ya ngoma yake mpya ‘Wewe’ ilikuja vipi?, na hapa Mwalimu anatusanua ,

“Maudhui makuu yanayolenga wimbo huo ni washikaji au watu ambao tunafanya kazi ngumu sana lakini tukiokota hela matumizi yetu yanakuwa ya kusahau kile ambacho tumetoka kukifanya, unakuta mtu yupo migodini achimba madini lakini akipata hela akiingia mtaani watu watakunywa na kufanya kila kitu alafu hela ikiisha anarudi tena chimboni hayo ndiyo yalikuwa maudhui yangu”. Anasema Kontawa

Kupitia hayo maelezo mafupi inaonesha kuwa mwanamuziki Kontawa ni kati ya wasanii ambao hawasahau washikaji wanaotafuta pesa kwa ugumu, na hii si mara ya kwanza kwa ngoma hiyo, bali imekuwa kawaida kwa Kontawa kuimba mistari ambayo inawahusu watu ambao wanajitafuta kwenye maisha na wenye maisha magumu kama vile ambavyo mistari ya ‘Dunga Mawe’, ‘Champion’ inavyosikika.

Wengi wamekuwa wakijiuliza hivi Tawa huwa anawaza nini hadi kuandika mistari ya aina hiyo lakini kupitia Mwananchi Scoop Tawa amefunguka na kueleza kwa undani kabisa , kwanza anasema kuwa mara nyingi hawezi kuandika wimbo kama hajisikii kufanya hivyo, akiwa na mood nzuri ya kutengeneza nyimbo ndiyo huandika.

Anasema Tawa , “kinachopelekea mimi kuandika mistari ya aina hiyo ni kwa sababu na mimi nimeishi maisha hayo kwa hiyo mara nyingi naimba maisha yangu yaliyopita na ya sasa hivi , naamini huwa najizungumzia mimi mwenyewe kwa hiyo uhalisia wa maisha yangu huwa unazungumzia maisha ya watu wengi sana”.

Haya hapa naimani mdau wa Mwananchi Scoop utakuwa umepata majibu ya maswali kuhusiana na mistari ya Kontawa lakini hatukuachana naye bado tuliendelea kutaka kufahamu mengi kuhusu maisha yake halisi na ya muziki wake kwa ujumla, kama ilivyo kawaida kwenye ngoma zake huwa na kionjo kisemacho “Mimi Nachekaga Tu” naimani wengi wamekuwa wakisikia ngoma ikianza bila kujua kwa nini kipo kwenye wimbo na kinamaana gani?.



Lakini kupitia mahojiano tuliyofanya na Tawa anafungua Code kwenye hilo anatuambia kwa nini anatumia maneno hayo.

“Mi nachekaga ni usemi ambao natumia ipi kwenye nyimbo nyingi ambazo natengeneza na wengi wanaijua, ni kwa sababu kipindi hicho kuna siku zamani sana ‘nilirekodi’ wimbo alafu nikajikuta kwenye mizuka ya kuimba kwa sababu wimbo una verse kali nikajikuta kabla ya kuimba nikapiga hiyo “Mi Nachekaga Tu” kwa hiyo source ilikuwa hiyo.

Nilikuwa na vibe ya beat kali producer akaiacha kwa hiyo kila tukisikiliza mtaani wakawa wanasema ni noma kwa hiyo kila wimbo nikawa naichapa.”

Kama ambavyo Kontawa alishindwa kuzuia hisia zake juu ya mapenzi mazito aliyonayo juu ya kujiunga na jeshi hadi kuomba nafasi, mkali huyo amezungumzia hilo na kudai kuwa soon watu wataona muendelezo wa kile ambacho alikuwa anataka kukifaya kwa hiyo watu wategemee kuona soldier msanii.

Hatuja malizaaa kivumbi leo Mwalimu anafungua code tu, mkali huyo awali zilizuka tetesi za kumuhusisha kwenye mapenzi na Zee Cute lakini sasa si tetesi tena kwani wmeamua kuweka wazi mambo yao.

Sasa basi Scoop tukataka kusikia neno lolote kutoka kwa Kontawa kwenda kwa mrembo Zee Cute.

Kontawa anasema “Zee Cute ni mwanamke mzuri, kwenye kumchagulia wimbo wa mapenzi asikilize namchagulia wimbo wangu ‘Mbalamwezi’ ambao nimefanya mimi na J Melody”.

Kontawa hakuishia tu kuusema wimbo huo bali aliimba kionjo chake kidogo, haha aisee fautani na mapenzi wewe.

Inafahamika kuwa Zee Cute ni mwanamuziki, tukataka kufahamu mwanamke ambaye Kontawa hawezi kuwa naye kwenye mahusiano , lakini alifunguka na kudai kuwa hawezi kudate na mwanamke ambaye kichwani hayupo smart, ambaye hawezi ku-control mambo yake , kwa hiyo ukiachana na uzuri lazima mwanamke awe smart kichwani, so dada yangu kama unasoma jarida hili jiulize kichwani upo smart na kama haupo smart jua kabisa Kontawa humpatiii.


Sifa nazo hakuacha kuzimwaga kwenye ngoma yake ya ‘Champion’ kwani umempa mafanikio mengi na imefanya awe msanii rasmi kwani mwanzo alikuwa field, bila kusahau kwenye upande wa kuomba support mkali huyo hakuliacha hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags