Mchezo wa rede unavyo endelea kupata umaarufu

Mchezo wa rede unavyo endelea kupata umaarufu

Na Asha Charles

Alooo weeeeee!! Its frieday na ramadhani ndo hiyooo kama inaanza kututupa mkono hivi, sasa basi kwenye segment yetu ya burudani na michezo leo tumekusogezea mchezo ambao wengi wetu sana tuliucheza utotoni.

Kama tunavyojua sasa hivi mchezo wa mpira wa miguu ndo umeshika kasi sana kuliko hata ile tulioizoea hapo awali, baadhi ya watu wamekuwa wakilalamikia kuhusiana na michezo ya asili kutotiliwa maanani.

Lakini si hvyo ni vile tuu haijapata watu wakuisponser ikaenda mjini, nikizungumza michezo ya asili nazungumzia bao, kipande nk.  Kwa wale wakishua kama tumewaacha kidogo simnajua tena hawa wenzetu lazima tuwaelekeze kidogo kidogo.

Nataka kuwajua wasioelewa Zaidi kuhusu mchezo huu, najua kunabaadhi ya watu watanishangaa kwanini naeleza kuhusu mchezo wa lede, kwani hukumbuki yule binti aliesema hajui kupika ugali acheni tuu haya mambo yapo bwana basi tuachane nayo tuendelee na mada yetu…

Rede ni mchezo asilia  wa kitamaduni unaochezwa na wanawake nchini Tanzania na nje ya bongo pia mchezo huu ni asili ya watoto wa Kiafrika ambao unaweza kuchezwa na watu kuanzia 3 nk.

Mchezo huu wawili wanazinga mmoja upande huu na mwingine upande mwingine, harafu mwingine anaka katikati harafu hurushiana mpira kwa kumlenga wa katikati.

Na huyo wa kati anakwepa kupigwa au huvizia kudaka mpira, kisha ampige nao mmoja wapo kati ya waliorusha, akifaulu kumpiga alama huongezeka na akifeli alama zinapungua akizembea kabisa basi kuya aga mashindano na kumpisha mtu mwengine nafasi yake mpaka apatikane mshindi. 

Kuna maneno ama lugha ina yotumika katika mchezo huu wa rede kama ilivyo katika michezo mingine maneno hayo kama stop, rede, hola, mpira tobo, babua, kuzinga, nk. 

yaani ukichimba kiundani utakuta mwaafrika alikuwa na michezo yake kadhaa aliyofanya tena nayo ilikuwa ikingiliwa na kubadilishwa mfano mieleka na shaba. Dah!! Sjui walikuwa wanafanyaje hawa majamaa hahahahahaha!!!! Tuyaache hayo twende kazi sasa yaani leo mpka kieleweke. 

Mchezo huu umeanza kuchezwa zaidi na wanawake kuanzia miaka 15nk, na ulianzishwa toka miaka ya 1990’s  ulikuwa unachezwa na wanafunzi shuleni lakini kuanzia mwaka 2000 mchezo huu umekuwa na mvuto zaidi na kuchezwa na watu wazima yaani  kila sehemu kwanzia mitaani viwanjani famasiala nini!!.

Huu mchezo bwana chanzo chake kikuu ni mtaani uswahilini kwetu kwa wale wenzetu washua wanaskia tuu kuna mchezo wa rede, tusiwalaumu ndo maisha hatuwezi kuyabadirisha.

Mchezo huu bwana unafaida kede kede kama vile kuupa mwili jasho pale unapokuwa unakimbia ni faida moja kubwa sana, unaburudisha na kujenga afya yako tuseme tu mchezo huu ni kama kufanya mazoezi tuu. Tuseme tuu unaburudika uku umaimarisha mwili. 

Na hizi ni baadhi ya aina za mchezo huu kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira kuna mpira wa miguu, bascketball, netball nk…

  • REDE YA CHUPA

Hii rede huwa ina mtu wa mwanzoni na mwishoni mchezaji huwa katikati na chupa yake inawekwa katika sehemu iliokuwa na mchanga kiasi, utakapo anza tuu mchezo huo atatkiwa kuijaza mchanga chupa kabla ya japigwa na mpiara (kubababuliwa ).

Endapo akapigwa na mpira kabla ya kujaza chupa mchanga basi atakuwa ameshindwa na hana budi kumpisha mchezaji mwengine aendelee kuchezaa.

  • REDE YA MSTARI KATI

Lakini rede hii inatofautiana kidogo na rede ya chupa yenyewe wachezaji huji gawa makundi mawili kisha huchora mstari kati ili kutofautisha baina ya kundi na kundi na kurushiana mpira timu itakayo shindwa itakuwa imeaga mashindano.

Aina nyinginezo ni rede ya vijiti, rede ya kuhesabu namba, kujificha, tobobao na mingine kibao.

Kwa Tanzania timu za rede amabazo zinafanya vizuri Zaidi ni ya Kwa Mkongo Queens ilioko Chamazi jijini Dar es salaam ndio mabingwa wa mashindano ya rede mstari kati maarufu kama T.O.K. REDE CUP.

Licha na taji hilo walilopata pia walishindana katika mashindano ya Mbunge wa Mbagala Abdallah Chaurembo maarufu kama CHAUREMBO REDE CUP na kutwaa ubingwa kwa mara nyingine tena.

Mpaka hapa tunaona jinsi gani rede imekuwa maarufu mpaka kufikia huko mbele umekuwa ukifatiliwa na watua warika zote na kupata wadhamini kufuatia mchezo huo, visiwani Zanzibar wana timu nyingi kutokana na miitikio mkubwa wa mchezo huo japo kuna kipindi cha kati mchezo huo ulipungua kasi.

Kocha mchezaji watimu ya rede ya Jamali Mafunda Ramadhani amesema yupo mbioni kwa kuandaa kampeni ya kuhamisha michezo uko Zanzibar hususani mchezo wa rede kwa wa sichana ili kuwasaidia kuwajenga kimazoezi wawe bize.

Mpaka imekuwa ndio chanzo kengine cha kukua kwa mchezo, imewasaidia watoto wakike kutokuwa na ma kundi mabaya ya mitaani na kuwa bize na michezo ya kitamaduni.

Kama tunavyoona mchezo huu kwasasa ni kama umekufa lakini bado kuna watu hawajaukatia tamaa kama vile michezo mingine, tunaamini ipo siku utafufuka kama ulivyokuwa hapo awali.

Ukiachana na hayo bwana kuna media mbalimbali nchini zimekuwa zikifanya mashindano ya rede uswashilini na kutoa zawadi mbalimbali kama vile, mbuzi, kuku na pesa tasrimu. Hii inaendelea kutupa hamasa kuwa mshezo huu iposiku utakuja kupata umaarufu kuliko watu wanavyofikiria.

Ooooooh! Tumewasogezea mada hii bwana kujua hali halisi ya michezo mingine ukiachilia mbali hiyo ambayo inafuatiliwa Zaidi, tunajua unajua mengi sana kuhusu mchezo huu lakini tupo hapa kukujuza zaidi 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags