Mchezaji Chucho amezwa na mamba

Mchezaji Chucho amezwa na mamba

Mchezaji wa ‘timu’ ya Deportivo Rio Canas kutoka nchini Costa Rica, Jesus Alberto Lopez maarufu kama Chucho (29) anadaiwa kufariki baada ya kumezwa na #Mamba mtoni alipokuwa akiogelea.

Kwa mujibu wa Mirror news imeeleza kuwa, tukio hilo lilimtokea wakati akiwa mapumziko ndani ya mto upatikanao katika jimbo la Guana Caste nchini humo.

Familia ya Lopez imetoa wito kwa umma kusaidia kuchangia gharama za mazishi ya mchezaji huyo, huku ‘kocha’ wa ‘timu’ yake, Luis Carlos Montes pia akiendelea kukusanya michango kutoka sehemu mbalimbali.

Chochu ameacha watoto wawili, ambao mmoja ana miaka nane na mwingine akiwa na miaka mitatu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags