Mcheza mpira Hernandez auawa kwa kupigwa risasi

Mcheza mpira Hernandez auawa kwa kupigwa risasi

Mchezaji wa ‘timu’ ya Taifa ya Panama, Gilberto Hernandez, ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji wa Colon, inadaiwa watu waliyokuwa na silaha walishambulia kundi la watu ambalo kati yao alikuwemo mchezaji huyo.

Hernandez alifariki dunia na watu wengine saba walijeruhiwa licha ya uchunguzi juu wa mauaji hayo bado unaendelea na bado haijajulikana kama watu hao walimlenga mchezaji huyo au laa.

mambo yamebadilika nchini humo hasa katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mauaji katika Mji wa Colon kutokana na mivutano inayodaiwa kati ya magenge mawili makubwa yanayogombania njia za usafirishaji wa dawa za kulevya, ikiwa mwaka huu pekee zaidi ya watu 50 wameuawa katika mji huo wenye wakazi takribani 40,000.

Aidha Shirikisho la soka la nchi hiyo na ‘klabu’ aliyokuwa akiichezea Hernandez wametuma salamu za rambirambi kwa familia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags