Mbwa wa Biden afukuzwa Ikulu

Mbwa wa Biden afukuzwa Ikulu

Mbwa wa familia ya Rais nchini Marekani, Joe Biden, Commander ametimuliwa Ikulu kwa kutoka na mfululizo wa matukio ya kuwang'ata wafanyakazi wa eneo hilo wakiwemo walinzi wa Rais huyo.

Taarifa za kuondolewa kwa mbwa huyo, zimethibitishwa na msemaji wa mke wa Biden, Jill Biden, Elizabeth Alexander.

Inaelezwa kuwa wiki iliyopita, mbwa huyo alimng'ata mmoja kati ya walinzi wa siri wa Biden na kusababisha apatiwe matibabu ya dharura.

Tukio hilo ni kati ya matukio 11 ya mbwa huyo kuwang'ata watumishi mbalimbali wa Ikulu nchini humo.

Msemaji huyo wa mke wa Rais alieleza kuwa Rais Biden na mkewe wanajali sana kuhusu usalama wa watu wanaofanya kazi White House na wale wanao walinda kila siku, Ingawa mpaka sasa hajajulikana ni wapi alipo mbwa huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags