Mbuzi azaa kiumbe kinachofanana na binadamu, Dodoma

Mbuzi azaa kiumbe kinachofanana na binadamu, Dodoma

Na Habiba Mohamed

Aiseeeeeee! Waswahili wanasema ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni Huko Mkoa wa Dodoma Kijiji Cha Itololo machinjioni wilaya ya Kondoa, wakazi wa Kijiji hicho washangazwa na tukio la mbuzi kuzaa kiumbe kinachofanana na binadamu ambapo mmiliki wa mbuzi huyo alifanya mahojiano kwa kina na kituo maarufu Cha habari na kufunguka na kusema

"Nimeshangazwa na tukio hili,mbuzi wangu amezaa watoto wawili  mmoja yuko salama na mwingine ndo huyu amezaliwa akiwa na baadhi ya viungo vya binadamu kama pua, masikio hata sura ikifanania kabisa na binadamu na huu ni uzao wake wa nne."amesema

Aidha mfugaji huyo aliendelea kwa kusema "baada ya kuona tukio hiloo nikawashirikisha na majirani zangu pia nashukuru hawakulipokea kwa namna ya tofauti sana juu yangu kwani ni vitu hutokea katika uzazi wa kiumbe chochote ni mipango ya Mungu." Amesema

Mmmmmmh! Dondosha comment yako ukitueleza mkasa gani ama tukio gani la kushangaza lilitokea katika jamii yako na hatua gani ulichukua dhidi ya tukio Hilo. Till next time byeeee






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags