Mbinu za kufanya betri la simu yako lidumu zaidi.

Mbinu za kufanya betri la simu yako lidumu zaidi.

Mambo niaje? Karibu kwenye ukurasa wa Smartphone na leo bwana bila kupoteza wakati nakuletea njia ambazo zitakusaidia betri la simu yako kudumu.

Nikwambie tu kuwa Matoleo mengi ya simu siku hizi yanakuja na betri ambazo wastani  wake hazidumu kwa zaidi ya siku tatu bila kuhitaji kuchajiwa tena, na mbaya zaidi kwa wateja wa internet  na wa kuangalia video wao hujikuta kila inapoitwa leo lazima wahitaji huduma ya kuchaji simu zao.

Najua jambo hili linavyokera bwana sasa twende moja kwa moja kwenye njia ambazo zitasaidia kupunguza tatizo hili.

Punguza kuwasha kioo cha simu yako kila mara.

Kwa wengi wetu, simu imekuwa ni zaidi ya ulevi, kiasi kwamba karibu muda wote simu ipo bize ikibonyezwa bonyezwa, wakati mwingine bila ulazima wowote wa kufanya hivo. Hivyo ukiweza kujizuia kuwasha mara kwa mara kioo cha simu yako na kibonyeza bonyeza simu yako, kutasaidia kutunza chaji na kulifanya betri lidumu na chaji kwa muda mrefu zaidi.

Weka simu yako katika mfumo wa safari ya ndege (airplane mode)

Pale unapokuwa huhitaji mawasiliano yoyote na huhitaji kuzima simu yako, basi ni vizuri kuweka simu yako katika mfumo huu, kwani husaidia kutunza chaji ya simu yako bila kulazimika kuzima simu.

Hakiba ya chaji.

Ikiwa unaweza kuwa na vifaa saidizi vya kukusaidia kutunza chaji, basi ni vizuri zaidi kuhakikisha vinakuwa na chaji ya kutosha kwani itakufaa pale utakapokuwa umeishiwa na chaji ya betri lako. Baadhi ya vifaa hivi ni pamoja na betri la simu la ziada, powerbank, na vingine vinavyoweza kuhifadhi chaji kwa matumizi ya badae.

Zuia vitoa taarifa

Simu nyingi zenye uwezo wa kutumia mtandao wa intaneti, zinahuduma ya utoaji wa taarifa kwa mawasiliano mbalimbali (push notifications), kama vile ujumbe uliopokewa wa whatsapp, facebook, instagram, barua pepe (email) na kadhalika. Kwa kuzuia vitoa taarifa kwanye mpangilio wa simu yako (phone settings) kutasaidia kutunza chaji ya betri lako na kuliwezesha lidumu na chaji kwa muda mrefu.

Punguza kutazama moja kwa moja video na mziki mtandaoni (streaming)

Ikiwa unapenda mziki na video, basi ni vizuri kutumia video na miziki iliyoko kwenye simu yako, na kuepuka kuisikiliza moja kwa moja toka mtandaoni. Unapotazama na kusikiliza sauti moja kwa moja toka mtandaoni kunatumia chaji nyingi ya betri hivyo kupukutisha kwa kasi akiba ya chaji yako.

Punguza kucheza gemu mtandaoni.

Michezo mingi ya gemu husaidia kutuliwaza na kuchangamsha ubongo, lakini pia ni ukweli kuwa magemu mengi hutumia chaji nyingi na kuharibu uimara wa betri. Yapo magemu mashuhuri kama vile ‘pokemon Go’ au ‘Candy Crush Saga’ mengineyo mengi ambayo hulazimu kuwepo kwa mawasiliano ya intaneti kwanza ndipo uweze kuyatumia.

Punguza mwanga wa simu yako (brightness)

Mwanga wa simu pia nao hutumia chaji nyingi ya betri la simu yako, na hususani ikiwa kioo cha simu yako ni kikubwa na mwanga ni mkali. Hivyo ni vizuri kupitia mpangilio wa mwanga wa simu yako na kuupunguza kwa kiasi ili kusaidia utunzaji wa chaji. Pia kumbuka kuzima mwanga wa simu unapokuwa huitumii ili kutunza chaji.

Endelea kutembelea magazine yetu ili uweze kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya Smartphone.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post