Mbappe athibitisha kuondoka PSG

Mbappe athibitisha kuondoka PSG

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Paris Saint-Germain (PSG), Kylian Mbappé, amethibitisha hadharani kwamba ataondoka katika ‘klabu’ hiyo ya ‘soka’ ya Ufaransa mwishoni mwa msimu huu.

Mbappe ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii ambapo alitoa shukrani kwa mashabiki na viongozi wa ‘klabu’ kwa kumsapoti wakati akiwa na PSG.

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali Mbappe anatarajia kujiunga na ‘klabu’ ya Real Madrid katika msimu mpya utakaoanza.

Mbappe alisaini mkataba wake wa kwanza mwaka 2017 akiwa na miaka 18 na kusaini tena mkataba mpya wa miaka miwili na timu hiyo 2021 huku takwimu zake zikiwa ni amecheza michezo 306, amefunga magoli 255 na kutoa Assists 108.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post