Mbappe amshitaki muuza kababu

Mbappe amshitaki muuza kababu

Mchezaji wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameripotiwa kumshtaki mmiliki wa duka linalouza kababu huko Ufaransa baada ya kutumia jina lake kwenye kutangaza biashara yake hiyo.

Mohamed Henni, ambaye ni mmiliki wa duka hilo la kuuza kababu aina ya Klub ambazo zinatengenezwa kwa mkate wa duara, amekua akitangaza kababu hizo kwa kueleza kuwa zinafanana na fuvu la kichwa cha Mbappe.

Ripoti zinadai ‘timu’ ya wanasheria wa Mbappe imemchukulia hatua za kisheria Mohamed wakiamini anachafua jina la staa huyo.

Henni, ambaye ana wafuasi milioni 1.8 kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo aliweka picha zilizokuwa zinaonyesha barua alizopokea kutoka kwa wanasheria hao.

Aidha kwa mujibu wa barua hizo zimemtaka Henni kuondoa jina la Mbappe kwenye menu yake ndani ya siku nane na akishindwa kufanya hivyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kutumia jina la staa huyo kwenye biashara bila ridhaa yake.

Hata hivyo, Henni alionekana kuipokea taarifa hiyo tofauti akisema Mbappe na wawakilishi wake wamekosa aibu kwa kumtumia barua hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post