Mbappe akubali kujiunga na Real Madrid

Mbappe akubali kujiunga na Real Madrid

Baada ya siku kadhaa nyuma kutangaza kuondoka katika ‘klabu’ ya Paris St-Germain (PSG) mshambuliaji Kylian Mbappe amekubali kujiunga na Real Madrid msimu mpya utakaoanza.

Nahodha huyo wa Ufaransa mwenye miaka 25 bado hajasaini mkataba na Real Madrid, lakini mkataba huo huenda ukatangazwa mara tuu itakapobainiaka kuwa Madrid na PSG hazitaweza kukutana kwenye ‘Ligi’ ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kwa mujibu wa BBC, Mbappe anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na ‘klabu’ hiyo, akipata €15m (£12.8m) kwa msimu, pamoja na ‘bonasi’ ya usajili ya €150m (£128m) ambayo atalipwa kwa miaka mitano.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags