Mayweather asaidia familia 70 zilizo athirika na moto

Mayweather asaidia familia 70 zilizo athirika na moto

Bondia wa zamani wa kulipwa Floyd Mayweather amejitoa kuwasaidia zaidi ya watu 70 waliokumbwa na athari ya moto kisiwani Hawaiian, baada ya baadhi ya watu kupoteza makazi na wengine wasiopungua 53 kufariki dunia.

Kwa mujibu wa MTZ news imeeleza kuwa bondia huyo amewapa msaada zaidi ya watu 70 waliokimbia makazi yao kutokana na moto huko Maui kwa kuwapatia sehemu ya kukaa, chakula na mavazi.

Baadhi yao amewalipia vyumba vya kulala katika Hotel kwa muda wa wiki kadhaa, pia inasemekana anasaidiana na H&M company kupata nguo kwa ajili ya watu wenye uhitaji.

Aidha Maywether amethibitisha kufanya jambo hilo kwa siri kwa sababu anahitaji kusaidia kwa moyo wake wote na sio ku-take attention kwenye vyombo vya habari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags