Mawazo ya biashara kwa mwaka 2023

Mawazo ya biashara kwa mwaka 2023

I hope mko pouwa wafuatiliaji wa Mwananchi Scoop, sasa leo bwana katika biashara tutakujuza mambo mbalimbali kuhusiana na biashara ambazo zinalipa zaidi kwa mwaka huu. 

Kama tunavyojua mwaka ndo kwanza unaanza kuchangamka yaani namaanisha haujachelewa sana kufanya maamuzi, sisemi uache biashara ulionayo na uanzishe ninayo kwambia hapana, bali chakufanya tuu unaweza kuongezea hapo hapo katika biashara yako au kuongeza tuu mtaji.

Biashara siku zote na muda wote tunaelekezana kuhusiana na kujitoa, heshima na lugha nzurii ka wateja wako. Haya sasa tunaenda katika mada yetu na leo tumesema tunazungumzia kuhusiana na mawazo mapya ya biashara kwa mwaka 2023 ambayo ukifanya moja kwa ufasaha litakupatia faida kuliko hata unavyofikiria…

  • Biashara ya urembo(kusuka,makeup,kucha)

Kwa mwaka huu biashara hii ya urembo imekuwa biashara ambayo ukiifanya inakupatia faida sana ndo maana watu wengi siku hizi wanajishughulisha nayo, mabinti wengi wa vuoni siku hizi wametokea sana kupenda urembo wa kucha, make up na kusuka kutokana na kupata muonekano mzuri mbele za watu.

 Hivyo basi ukifanikiwa kufungua biashara hii karibu na chuo utakuwa umetoboa sana, kwasababu biashara hii huwezi kulala njaa na kwa makadirio ya wateja ni kuanzia 10 na kuendelea. 

  • Biashara ya kupika kwa oda.

Pili ni hii ya kupika chakula, siku hizi bwana wabongo wengi wamebadilika sana, siku hizi wanaishi maisha wanayoishi watu wa nje kutokana na kutokupoteza muda. 

Siku hizi watu wanajari sana muda wao wewe kama mfanyabiashara hii ni fursa yako ya kupikia watu kwa oda na itakulipa Zaidi ya ulicho tarajia.

Watu wengi siku hizi kwanza ni wavivu kupika, pili uchovu wa kazini nk. So mtu anaona bora aagize chakula tuu ale na maisha mengine yaendeleee. 

Fanya utafiti wa soko ili kujua watu wanapenda kula nini wakati wa chakula cha mchana/usiku na ni kiasi gani wako tayari kutumia kisha tengeneza menu yako na bei, wala usisumbuke kufikiria wateja wa mbali anza na maeneo ya karibu na wewe. 

Pika kwa kiwango vihavyohitajika usafi kuanzia vyombo na muonekana wa mleta chakula ni jambo kuu kwenye biashara ya chakula, mapishi na matunda kidogo huongeza wateja wa uchumi mdogo na wa kati.

Nimekumbuka kama unavyojua kipindi hichi cha ramadhani watu wengi wanashinda maofisini kutoka wanachelewa sana so unaweza kupika futari na kuuza kwa oda kwa watu walio maofisini, cha kufanya ni kutafta ofisi kama tatu au hata tano na kuanza kuchukua oda kwa wanaohitaji.

  • Biashara ya kuuza maua 

Kusema ukweli siku hizi bwana wabongo sijui tumeadapt mambo za wazungu yaani siku hizi tumekuwa na mapenzi na maua mno, mtu akikuletea zawadi ya maua unaona kama dunia yote ni yako peke yako unajiona ndo unapendwa Zaidi. So biashara ya maua kwa Tanzania sasahivi inalipa sana.

Na watu huitimia kwenye birthiday, mahari, misiba, na sherehe mbalimbali, kama tunavyojua shughuli kama hizo kila siku zinafanyika yaaani kila siku watu wanazaliwa watu wanapelekeana zawadi.

So biashara nyingine ambayo itakupatia faida Zaidi ni hii niamini kwasababu nimefanya uchunguzi na nimeliona hilo, cha kufanya wewe ni kuwa karibu na wanaofanya biashara hiyo ili wakuelekeze biashara inavyokuwa, na kukupa mfano tuu ua moja si chini ya shilingi elfu 10 na kuna hadi ya Laki moja so niwewe kufanya maamuzi.

  • Biashara ya saluni ya kiume

Biashara ambayo watu wengi wanaizarau ni hii lakini ukipata sehemu yenye mzunguko wa wawatu utakuja kuamini ninachokizungumza, niashawahi kukutana na mtu mimi akaniuliza hivi hii biashara inafaida kweli ni kamjibu hakuna biashara iaio na faida.

Ukitaka kujua biashara hii inafaida sana siku hizi nenda katika saloon ambazo wanatengeneza nywele za dread ( kusokota nywele) au kwa jina lingine  kuongeza nywele hii biashara inalipa sana na mara nyingi hufanywa katika saloon za wanaume so biashara hii kwa mwaka huu imekuwa ni yakipekee sana na yenye faida isiyo tarajiwa.

Mfano kichwa kimoja cha kukisokota ni shilingi elfu 25 mpaka 30, kwa siku wakija watu wa 5 unaendesha maisha yako bila wasiwasi. 

  • Biashara ya kutembeza watalii.

Kama tunavyojua kusomea tourlism ni miezi 3 mpaka 6 na inaweza kukulipa zaidi ya hiyo ada uliotoa kwa miezi. Siku hizi watu wa mataifa mbali mbali wanafika katika vivutio mbali mbali kwa ajili ya utalii na hii inakupatia faida ya kujuana na watu wa mataifa mbali mbali. 

Cha kufanya ni kutafuta ada na kwenda kusoma hiyo course kwasababu itakuja kunufaisha sana, nahii inapendeza sana sana ikafanywa na vijana ambao age yao bado haijakimbia sisemi mtu mzima usifanye laaahashaa! Kwako wewe nahofia familia ko ukichagua biashara chagua ambayo itakupa uhuru wa kuifanya bila kuingilia maisha yako binafsi.

Alooooh! Sijui niwaambie wiki ijayo nashuka na mzigo gani au niwaache kidogo, so natumai kabisa kwa mada ya leo huwezi kuondoka patupu lazima kuna kitu utakuwa umekipata, usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop kwaajili ya kujifunza Zaidi….


 







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags