Mavokali afunguka kisa kizima gari yake kupasuliwa vioo

Mavokali afunguka kisa kizima gari yake kupasuliwa vioo

Hellow! Kama kawaida yetu Mwanachi Scoop huwa hatunaga jambo dogo, basi bwana kumekuwa na sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii baada ya msanii Mavokali kushare video katika instastory yake ikionesha namna gari yake aina ya BMW lilivyopasuliwa vioo na watu wasiojulikana.

Basi team ya Mwananchi Scoop hatukulifumbia macho suala hili tukaamua kumvutia waya kijana huyo ili atueleze kiundani kuhusiana na tukio zima lililotokea na kueleza ishu yote.

“Tatizo hili limenipata usiku wa kuamkia jana nyumbani kwangu, mimi nilitoka gari niliacha nyumbani narudi nakuta limepasuliwa vioo na mtu aliefanya tukio hilo mpaka sasa sijamfahamu bado” amesema Mavokali

Kupitia mitandao hiyo hiyo ya kijamii baadhi ya watu wameonekana kutilia shaka na tukio hilo na kusema labda msanii huyo anataka attention kwa ajili ya kazi yake mpya, lakini mwamba huyo amaefunguka na kusema;

“No unajua Watanzania washazoea kuwa kila msanii anapotaka kutoa wimbo basi ataambatanisha na tukio ili iwe kiki ya kusukuma wimbo, ila kwangu haipo hivyo kwa watu wanao nifahamu nimekuwa ni mtu nisiependa kiki sababu mashabiki wangu wanataka mziki wangu na sio kiki na isitoshe tukio limenifika kweli” amesema Mavokali

Kulikuwa na tetesi kupitia social media zikisema kuwa tukio hilo eti limetendwa na mume wa mtu ikimaanisha kuwa anadate na mke wa mtu mwamba akafunguka kuhusiana na tuhuma hizo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusiana na suala hilo, na ameshalifikisha katika ngazi za juu kwa uchunguzi zaidi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post