Mavazi ya wanaume yanayowavutia wanawake

Mavazi Ya Wanaume Yanayowavutia Wanawake

Ni siku nyingine tena tunakutana kupitia safu hii, tumekuwa tukijuzana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya mitindo, urembo na mavazi ambayo najua huenda unayajua ila mimi nakujuza tu zaidi.

Leo tutaangalia aina mbalimbali ya mitupio kwa wanaume ambayo hupendwa zaidi na wanawake.

Wataalamu wa mambo ya mitindo wanawaelezea wanawake kama ni watu wanaopenda sana kuvaa na kupendeza japokuwa sio wote ila kwa asilimia kubwa wanajitahidi kwenye kutupia.

  1. TSHIRT NA JEANS 

Moja ya mavazi ambayo wanawake wengi wanapendelea wanaume wavae ni jeans na t- shirt. Kama mwanaume akipangilia vazi hili vizuri basi muonekano wake utakuwa wa kuvutia na nadhifu muda wote na utawavutia wanawake wengi.

  1. JEANS NA SHATI

Aina nyingine ya mavazi ni pale mwanaume anapovaa jeans kali akiwa na shati ambalo juu yake anaweka koti la suti huku chini akiwa amevaa raba au viatu vingine vizuri, hakika mavazi hayo pia uwavutia wanawake.

  1. SUTI

Pia lipo vazi la suti, hapa kama mwanaume akishona au kununua vazi hili na kisha kuchagua rangi inayopamba na kuendana na ngozi yake pamoja na kupangilia, ataonekana nadhifu na wa kuvutia.

  1. KITENGE SHIRT NA SURUALI

Aina nyingine ni pale wanaume anaposhona shati la kitenge na kuvalia na suruali inayoendana na rangi ya kitenge hicho, hakika vazi hili linapopangiliwa vizuri huonekana la kuvutia sana.

  1. T-SHIRT NA SHORTS

Vilevile lipo vazi la shorts na t-shirt. Vazi hilo nalo ni zuri na wanawake wengi hupenda wanaume walivae hasa katika siku za mapumziko au pindi wanapokwenda ufukweni.

Ikumbukwe kuwa katika mavazi yote haya ili kuonekana nadhifu ni muhimu yakawa safi na yaliyopangiliwa vizuri.

Natambua lipo tatizo la wanaume wengi kushindwa kwenda na wakati kwa kuvaa mavazi yanayovutia hivyo kupitia safu hii ya leo najua watakuwa wamejifunza kitu. Tukutane tena siku nyingine.

 

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post