Mavazi ya Stara Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Mavazi ya Stara Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Habari msomaji wetu, ni siku nyingine tunakutana tena kujuzana mambo mbalimbali ya urembo, mitindo, mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujuza zaidi.

Leo nitakujuza mavazi ambayo mwanamke na wanaume waislamu wanapaswa kuyavaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wote tunafahamu kuwa Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni moja ya nguzo tano za dini ya kiislamu ambapo kwa siku 29 au 30 kuanzia April 03, mwaka huu kwaislamu wote walianza mfungo wao.

Katika mfungo huo pamoja na kujizuia kula chakula na maji kwa asubuhi na mchana, pombe, sigara, kutoa kauli chafu au kuzungumza uongo, pia yapo mavazi ambayo mwanamke wa kiislamu na wanaume wanapaswa kuyavaa au upendelea zaidi kuvaa.

Kwa sasa ukitembea mjini utakuta wanawake wengi wamevalia mabaibui au magauni marefu yaliyofunika mwili wao huku wanaume wengi wakiwa wamevalia kanzu.

Hata hivyo wadadavuzi wa mambo wanasema kuwa kwa hakika mavazi hayo ya stara wanayovaa wanawake uwapendeza sana hivyo wanatamani wangekuwa wakiyavaa wakati wote si tu katika mwezi huu mtukufu.

 

Wanasema kama wanawake wote wangekuwa wanavaa hivyo kipindi chote basi vizazi vijavyo visingekuwa vikivaa mavazi ambayo hayapendezi katika jamii.

Hata hivyo inaelezwa kuwa mavazi hayo ya stara yanampa mwanamke heshima, kujiamini, kuwa na mvuto na kumfanya apendeze zaidi.

Hapa hatusemi uongo ebu tuambie hata wewe unayesoma safu hii mavazi haya hayawapendezi kweli wanawake na kuwafanya wajiamini. Hilo ni swali nimekupa na utajijibu mwenyewe.

Kwa sasa, hata wanawake ambao si Waislamu ununua mavazi ya stara na kuyavaa katika kipindi cha Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Wanawake wengi ununua mavazi hayo ya stara kutoka kwa wabunifu wa mavazi wa ndani yaani hapa nchini na hawaagizi kutoka nje kama ilivyokuwa zamani, hususan kutoka nchi za Kiarabu.

Hapo zamani watu wengi walikuwa wakiagiza mavazi hayo ya stara kutoka nchi za Kiarabu lakini sasa hivi wabunifu wetu wa mavazi wamekuwa wakitengeneza kwa wingi.

Kwa leo napenda kuishia hapo na nawatakia mfungo mwema wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ‘Ramadhani Kareem’.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags