Mauzinde akatwa masikio na kutelekezwa msituni

Mauzinde akatwa masikio na kutelekezwa msituni

Hussein Abdala maarufu Mauzinde (30), mkazi wa Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi, amekatwa masikio yote mawili na watu wasiojulikana kisha wakamtelekeza msituni.

Inadaiwa kuwa tukio hilo limetokea jana Jumapili Juni 2, 2024 usiku eneo la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Watu hao baada ya kutekeleza uharifu huo, walimfunga bandeji kichwani na kumtelekeza kwenye Msitu wa Hifadhi wa Kibele.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa simu leo Jumatatu Juni 3, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Daniel Shila amesema atalitolea maelezo zaidi tukio hilo baadaye kwa kuwa yupo kwenye msafara wa viongozi.

"Kweli tukio hilo lipo, ila nitalitolea zaidi ufafanuzi baadaye kwa sasa nipo kwenye msafara wa viongozi," amesema Kamanda Shila.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags