Mauaji ya wakulima na  Wafugaji: IGP aagiza askari wapishe uchunguzi

Mauaji ya wakulima na Wafugaji: IGP aagiza askari wapishe uchunguzi


IGP Camillus Wambura ametoa maagizo hayo baada ya Watu wawili kuuawa na wengine wawili kujeruhiwa kutokana ya Polisi kutumia silaha za moto wakati wakizuia vurugu katika Kijiji cha Ikwambi, Wilaya ya Kilombero, Morogoro Oktoba 23, 2022

IGP Wambura amesema “Nimeunda Tume Huru kuchunguza vurugu zinazotokea, lengo ni kujua nguvu iliyotumika kudhibiti kama iliendana na uhalisia. Askari wote waliohusika wakae kando na ikibainika kuna uzembe au mapungufu hatua za kisheria zitachukuliwa.”

Awali, ilidaiwa baadhi ya wananchi walichoma moto ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Mofu na kusababisha vifo vya Watu wawili sababu ikiwa ni kutoridhishwa na maamuzi ya Viongozi wakati wa utatuzi wa migogoro ya Wakulima na Wafugaji






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags