Matendo ya R.Kelly yamchukiza binti yake

Matendo ya R.Kelly yamchukiza binti yake

Mtoto wa mwanamuziki R. Kelly, Joanne Kelly amepanga kuachia filamu fupi (Documentary) itayoeleza matendo ya unyanyasaji yaliyokuwa yakifanywa na baba yake.

Kupitia filamu hiyo iliyopewa jina la ‘R. Kelly’s Karma: A Daughter’s Journey’ imepangwa kuoneshwa Oktoba 11, 2024 katika chaneli ya TVEINetwork ambayo itajumuisha mahojiano na Joanne pamoja na mke wa zamani wa mwimbaji huyo, Drea, na mwanaye Robert Kelly Jr.

“Kwa muda mrefu, sikutaka hata kuamini kwamba ilitokea. Sikujua kwamba hata kama alikuwa mtu mbaya, angeweza kunifanyia kitu. Ninahisi kweli kwamba sekunde moja tu kabisa ilibadilisha maisha yangu yote.

“Hakuna mtu anayependa kuwa mtoto wa baba ambaye yuko hapa nje akiumiza wanawake na watoto,” amesema

Ikumbukwe Kelly sasa yupo gerezani anatumikia kifungo cha miaka 30 baada ya Septemba 2021, kukutwa na hatia ya makosa tisa yakiwemo ya ulaghai na ulanguzi wa ngono dhidi ya watoto chini ya umri wa miaka 15.

Kelly amewahi kutamba na ngoma kama Step in the Name of Love, Bump n' Grind, The Storm Is Over Now, Legs Shakin' na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags