Mastaa wa bongo waige mahusiano ya Navykenzo

Mastaa wa bongo waige mahusiano ya Navykenzo

Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii wa Bongo kutokuwa na mahusiano ya kudumu hii imekuwa ikiwaogopesha, watu wengine kuingia kwenye mahusiano na wasanii au watu maarufu kwa kuogopa kuumizwa au mahusiano kuishia kati.

Wakati mwingine unaweza kusema au ni kutokana na watu maarufu kufahamiana na watu wengi zaidi ndiyo maana akiwa katika mahusiano hata akifanya jambo liwe baya au zuri linafahamika kwa haraka, skendo kwao imekuwa kawaida na ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Inafahamika kuwa katika mahusiano siyo kila siku wahusika huwa na furahi wakisherekea maisha, hapana kuna siku za kupitia magumu tena yakuvunja moyo. Mfano alisi ipo kweye jamii zinazo tuzunguka kwa mke, mume au wapenzi kukwazana.

Aika na Nahreel maarufu kama Navykenzo, hawa ni moja kati ya wasanii waliodumu kwa muda mrefu katika mahusiano na kubahatika kupata watoto wawili wa kiume Tanzanite na Jamaica.

Aika na Nahreel walianza mahusiano yao tangu wanasoma wakiwa nchini India, wamekuwa pamoja na kushirikiana katika harakati zao mpaka walivyoingia kwenye muziki wakiwa na zaidi ya miaka 15 sasa.

Licha ya kuwa katika mahusiano kwa muda mrefu lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna taarifa zao za kufunga ndoa, lakini wapo pamoja wakishirikina pia kufanya kazi yao ya muziki.

Licha ya kutokuwepo kwa taarifa zao za kufunga ndoa utakumbuka mwaka 2019 waliulizwa na moja ya chombo cha habari nchini, kuwa siku gani watafunga ndoa lakini majibu yao hayakuweza kufafanua kuhusu ndoa yao. Walijibu,
“Nyinyi mtajuaje kama ndoa haipo labda tumeshafunga, halafu hakuna mtu ambaye amewahi kutuuliza hilo swali, watu wanauliza ndoa lini labda kwa sababu hatujaweka mitandaoni ila kwa ajili ya Watanzania tutatangaza hivi karibuni tutaweka tarehe na location". Walisema

Baada ya hapo hakukuwa na taarifa nyingine tena kuhusiana na ndoa yao huenda ni kwa sababu wawili hao wameamua kutoweka wazi maisha yao binafsi mitandaoni, licha ya kuwa ni watu maarufu.

Mafanikio yao wakiwa katika muziki
Nahreel pamoja na Aika walianzisha kundi lililoitwa Navy Kenzo ambapo mpaka sasa wanaitwa hivyo, walipata umaarufu mkubwa kupitia wimbo wao wa tatu ‘Chelewa’ uliotoka mwaka 2016 baada ya kuvunjika kundi lao la ‘The Industry’ mwaka 2014 ambalo lilikuwa na wasanii Aika, Wildad na rapper Rosa Ree.

Pia kupitia kundi lao wakiwa wawili waliweza kutengeneza vibao vingine kama ‘Kamatia Chini’, ‘Game’ ambayo ilikuwa kolabo na Vanessa Mdee, ‘feel good’ kolabo kati ya Wildad, ‘Lini’ kolabo na Alikiba, ‘Morning’ ndiyo wimbo wa kwanza katika albamu yao ya kwanza kabisa .

Kundi hili lilifanikiwa kutoa albam ya kwanza ya 'ABOVE IN A MINUTE’ iliyowashirikisha wasanii wakubwa barani Afrika kama Patoranking, Alikiba na Vanessa Mdee baada ya hapo waliweza na wanaendelea kutoa nyimbo nyingi na zinafanya vizuri mapaka sasa.

Pia wamefanikiwa kuwa na Academy ya kuwaanda watoto kwa ajili ya soka baadaye ‘Navykenzo Academy’ ambayo wanachukua watoto kuanzia miaka 3 mpaka 17 wanafundishwa michezo mbalimbali kwa ajili ya kuwa wanasoka wazuri baadaye.

Aika na Nahreel walianza mahusiano ya kimapenzi mwaka 2008 na mwaka 2018 waliweza kuadhimisha miaka 10 ndani ya mahusiano ya kimapenzi katika fukwe za Visiwani Zanzibar ambapo mpaka sasa wana miaka 15 katika mahusiano yao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags