Mashambulizi ya mashabiki kwa Diamond, Alikiba aingia kati

Mashambulizi ya mashabiki kwa Diamond, Alikiba aingia kati

Baada ya mtu mzima #Diamond kupata mashambulizi ya ku-copy asilimia kubwa ya nyimbo za wasanii wengine kutoka nje ya nchi, #Simba hakutaka kulikalia kimya swala hilo, na kuanza kujibu mashambulizi aliyokuwa akiyapokea.

“Niko angani TORONTO CANADA nasikia huko duniani kila chumba , club, chochoro na kona ya mitandao gumzo ni ‘Enjoy’, hayo mengine niachie mie ukisikia mtoto anapiga kelele ujue bakora imemuingia

Wakifanya wengine, utasikia ma-genius wana akili wame-sample, tukifanya sie tume-copy! Wangekuwa wanaumiza vichwa kweli wangeimba mangaka, lizombe au linguchumu ngoma na muziki ya kwetu mbona wameenda kudandia amapiano, tena za kuandikiwa.”

Kupitia ujumbe huo wa Diamond, mwanamuziki Alikiba naye hakukaa kimya aliibuka upya na kuwajulisha mashabiki wake ujio mpya wa ngoma yake itakayotoka mwezi ujao, huku akiongezea kwa kijembe kisemacho “kivunge cha mtozi tukitumie tutoe ngoma ya kiasili”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags