Mashabiki wenye hasira wa ‘timu’ ya Ajax, Waharibu uwanja

Mashabiki wenye hasira wa ‘timu’ ya Ajax, Waharibu uwanja

Nchini Holanzi mchezo wa ‘Ligi’ kuu kati ya ‘timu’ ya #Ajax waliocheza nyumbani dhidi ya ‘klabu’ ya #Feyenoord, ulisitishwa siku ya Jumapili, baada ya vurugu za mashabiki waliorusha fataki uwanjani.

Aidha hali hiyo ililazimu polisi wa kuzuia vurugu nchini humo kuchukua hatua za kisheria kuzuia ghasia hizo kwa kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki walio hudhuria ‘mechi’ hiyo.

Licha ya ‘mechi’ hiyo kusimama mara mbili, kutokana na moshi wa fataki zilizowashwa na mashabiki wa ‘klabu’ ya Ajax wakati ‘klabu’ ya Feyenoord wakiwa mbele kwa bao 3-0 katika uwanja wa Johan Cruyff Arena nchini humo.

Ghasia ilivyozidi kuwa kubwa kikosi cha polisi wa Farasi, kilijaribu kuwatawanya mashabiki wenye hasira kali waliokuwa nje ya uwanja wakifanya vurugu na kuharibu uwanja huo.

Ajax, wanashika nafasi ya 13 baada ya kuanza vibaya msimu huu wakishinda ‘mechi’ moja katika ‘mechi zao nne za kwanza za ‘ligi’, kitendo kilichoibua hasira kali za mashabiki ambao hawajazoea kiwango hiko kibovu kwenye ‘soka’.

Kutokana na matokea hayo kwa upande wa ‘klabu’ hiyo inadaiwa imechukua uamuzi wa kumtimua aliyekuwa mkurugenzi wa michezo, Sven Mislintat, licha ya kutokuwa na muda mrefu katika ‘timu’ hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags