Mashabiki wauawa, Mechi yaahirishwa

Mashabiki wauawa, Mechi yaahirishwa

Mchezo wa kufuzu #Euro2024 kati ya wenyeji Ubelgiji na Sweden umeshindwa kuendelea kipindi cha pili baada ya mashabiki wawili wa #Sweden kushambuliwa kwa risasi na kuuawa katika mji wa Brussels jana.

Inadaiwa mshambuliaji wa tukio ambaye bado hajakamatwa anahusishwa na kundi la #ISIS na inadaiwa alifanya hivyo ili kulipa kisasi tukio la kijana wa #Palestina kuuawa nchini Marekani hivi karibuni.

Wakati mchezo ukiahirishwa kwenye uwanja wa King Baudouin, matokeo yalikuwa sare ya 1-1, ambapo mashabiki walitakiwa kubaki uwanjani kwa saa mbili zaidi wakati ukaguzi ukiendelea kwa kuwa wanausalama wamehusisha tukio hilo na ugaidi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags