Mashabiki wanne wa Namungo wafariki, 16 wajeruhiwa

Mashabiki wanne wa Namungo wafariki, 16 wajeruhiwa

Uongozi wa ‘klabu’ ya Namungo FC umetoa taarifa ya gari walilokuwa wanatumia mashabiki wa ‘timu’ hiyo kutoka Ruangwa kuja Dar es Salaam kuishangilia ‘timu’ yao ikicheza dhidi ya Yanga ‘mechi’ ya Ligi Kuu leo Septemba 20 saa 1:00 usiku, limepata ajali eneo la Miteja karibu na Somanga mkoani Lindi.

Uongozi huo umesema mashabiki wanne wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa, wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi wilayani Kilwa kupatiwa matibabu.

"Uongozi tunatoa pole kwa Wanaruangwa, mashabiki, familia na kwa wote waliopata ajali hiyo," imeeleza taarifa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags