Mashabiki wamjia juu ‘Kocha’ kwa kumcheza Saka akiwa majeruhi

Mashabiki wamjia juu ‘Kocha’ kwa kumcheza Saka akiwa majeruhi

Inadaiwa kuwa mashabiki wa ‘klabu’ ya Arsenal wamemjia juu ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo Mikel Arteta baada ya kumchezesha mchezaji #BukayoSaka katika ‘mechi’ ya ‘Ligi’ ya  Mabingwa Ulaya dhidi ya #Lens wakati akiwa majeruhi.

Pamoja na ‘kocha’ huyo kuweka wazi hali ya mchezaji huyo baada ya kutolewa nje wakati ‘mechi’ ikiendelea huku Arsenal ikipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Lens, ndipo mashabiki wao walichukizwa kwani ‘winga’ huyo hakuwa ‘fiti’.

Mashabiki walishindwa kujizuia wakimtupia lawama Arteta kwani ‘winga’ huyo alikuwa ana jeraha ambalo linamsumbua kabla ya ‘mechi’ hiyo ya ‘Ligi’ Mabingwa Ulaya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags