Mashabiki wamchangia Ally Kamwe million 1

Mashabiki wamchangia Ally Kamwe million 1

Ni masaa machache tangu ‘bodi’ ya ‘Ligi’ Tanzania kumpiga ‘faini’ ya million 1,  Afisa wa habari wa ‘klabu’ ya Yanga, Ally Kamwe kwa kosa la kumkejeri mwamuzi Tatu Malogo, Kamwe ameweka wazi kuwa ameshachangiwa pesa hiyo na mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ally Kamwe ameweka wazi kuhusu taarifa hiyo kwa kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwa mahaba waliyomuonesha ya kumchangia kupitia ‘kampeni’ iliyoendeshwa na shabiki Jimmy Kimdoki ili kumuwezesha kulipa ‘faini’ hiyo kwa wakati na kuendelea na majukumu yake.

 Aidha Kamwe ameeleza kuwa amepokea adhabu hiyo kama njia ya Mungu kutaka kuzungumza naye, kwani kupitia adhabu hiyo ameona, kusikia na kujifunza mengi, kikubwa ameuona upendo wa dhati wa mashabiki wa Yanga kwake na amewashukuru kwa kuweza kumchangia kiasi hicho cha pesa.
.
.
#MwanachiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags