Mashabiki wakosoa sanamu la The Rock

Mashabiki wakosoa sanamu la The Rock

Ikiwa ni kawaida kutoka katika jumba la makumbusho la Grevin Paris nchini Ufaransa kuweka sanamu za watu maarufu mbali mbali, kwa mwaka huu imekua tofauti baada ya mashabiki kukosoa sanamu la muigizaji The Rock.

Mwaka jana jumba hilo la makumbusho lilitangazia umma kupiga kura ni mtu gani mashuhuri awepo kwenye maonyesho hayo ambapo orodha ya watu maarufu ilipendekeza majina ya wasanii kama.

Ariana Grande, Tom Holland, Zendaya, Dua Lipa, Elon Musk, Selena Gomez, Chris Pratt na Margot Robbie. Hivyo basi muigizaji The Rock alipata kura nyingi na kupelekea sura yake ndio itumike kwa ajili ya maonyesho ya mwaka huu.

Kufuatia na mashabiki kutoka mtandao wa X wamekosoa sanamu hilo katika sehemu tofauti tofauti ambapo wengine walisema sanamu hilo halifanani na muigizaji huyo, na wengine wakikosoa macho, mdomo huku baadhi yao wakisifu sanamu hilo.

Mshindi huyo wa WWE miaka ya 2000 anajulikana kupitia filamu mbali mbali kama vile Jumanji the next level, fast and furious, pain & gain nk.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags