Mashabiki waanza kuongea lugha moja na Messi

Mashabiki waanza kuongea lugha moja na Messi

Mshambuliaji kutoka #Argentina, #LionelMessi ameanza kubarizi kwa kujichanganya na raia wa Marekani, baada ya kuonekana akinunua bidhaa mbalimbali kwenye Supermarket jijini Miami.

Mwanasoka huyo hakusita kupiga picha na baadhi ya mashabiki wake waliokuwa katika Jimbo la Sunshine nchini Marekani, wakati akiwa anatoka kwenye Supermarket hiyo.

Ingawa Messi alitarajiwa kusaini mkataba wake na kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Miami siku ya Alhamisi, lakini utambulisho wake umechelewa, huku siku ya Ijumaa ikiripotiwa kama siku rasmi ya utambulisho wa mshindi huyo wa kombe la Dunia nchini Qatar.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags