Mashabiki Sudani Kusini walivyofuatilia mchezo dhidi ya USA, Olimpiki 2024

Mashabiki Sudani Kusini walivyofuatilia mchezo dhidi ya USA, Olimpiki 2024

Mashabiki wa michezo Sudan Kusini usuku wa kuamkia leo walikusanyika katika eneo moja kwa ajili ya kufuatilia mchezo wa Mpira wa Kikapu ambao ulishuhudia timu yao ikicheza dhidi ya Marekani ‘USA’.

Katika mchezo huo timu ya kikapu ya Marekani imeibuka na ushindi wa pointi 103 - 86 dhidi ya Sudan Kusini katika mechi ya Olimpiki huko Ufaransa.

Sudan imeshindwa kufua dafu mbele ya Marekani yenye mastaa kama Kevin Durant, LeBron James, Anthony Edwards, Devin Booker and Derrick White, Steph Curry na wengine.

Katika mechi hiyo Sudan Kusini imefanikiwa kushinda raundi ya tatu na pointi 21 kwa 18 huku raundi zingine tatu Marekani ikiibuka kidedea.

Ushindi wa Marekani katika mechi za kundi C umeipa nafasi ya kusonga hatua inayofuatia ikiwa kileleni na pointi 4 ikifuatiwa na Serbia yenye pointi 3 na Sudan Kusini yenye pointi 3 kila timu ikicheza mechi mbili, Puerto Rico inashikilia mkia kwenye kundi hilo baada ya kupoteza mechi zake zote mbili.

Mchezo wa mapema wa kundi hilo Serbia iliibuka na ushindi wa pointi 107 - 66 dhidi ya Puerto Rico.

Huu ni ushindi wa pili kwa Marekani baada ya mchezo wa ufunguzi dhidi ya Serbia kuibuka na ushindi wa pointi 104-84, ambapo Kevin Durant alifunga pointi 23.

Sudan ilifanikwa kushinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya Puerto Rico kwa pointi 99 - 79, Julai 28, mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags