Mashabiki Nigeria wa-report akaunti ya Grammy

Mashabiki Nigeria wa-report akaunti ya Grammy

Baada ya ugawaji wa Tuzo kubwa za Grammy kuwatosa Ma-staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, mashabiki kutoka nchini humo wamechukizwa na kitendo hicho na kuamua kui-report 'akaunti' ya Instagram ya Grammy huku wakidai kuwa hawakutenda haki kwa wanamuziki hao.

Kufuatiwa na video zinazoendelea kusambaa mitandaoni zimewaonesha vijana hao wakiwa na simu zao waki-report ‘akauti’ hiyo kutokana na wasanii waliowatarajia kuondoka na ushindi mnono, kushindwa kuchukua tuzo hizo.

Ma-staa ambao walifanikiwa kutajwa katika vipengele kadhaa kwenye tuzo hizo ni Burna Boy, Davido, Asake na wengineo lakini wote hao hawakuweza kuondoka na tuzo yoyote siku hiyo.

Tuzo za Grammy zilitolewa usiku wa kuamkia jana Febriari 4, nchini Marekani katika ukumbi wa ‘Crypto’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags