Mashabiki Euro wazuiwa kuingia na vitu hivi viwanjani

Mashabiki Euro wazuiwa kuingia na vitu hivi viwanjani

Kuelekea michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza kupigwa kesho nchini Ujerunani mashabiki wamepigwa marufuku ya kuingia na baadhi ya vitu viwanjani, kama vinywaji, vyakula, matunda na sigara.

Si hivyo tu pia kwenye pande wa ushangiliaji, mashabiki wamezuiwa kuingia na moto, fataki, filimbi, vuvuzela na Bendera ya chama cha aliyewahi kuwa kiongozi wa nchi hiyo, Adolf Hitler ‘Nazi’, pamoja na kutoruhusiwa kuingia na nyenzo kama vile bendera zinazounga mkono upande wowote wa mzozo unaoendelea huko Gaza kati ya Israel na Palestina.

Maelekezo ya kutoingia na vitu hivyo yametolewa na Shirikisho la Soka Barani Ulaya na yatafanyiwa kazi kwenye viwanja vyote 10 vitakavyotumika kuandaa mashindano hayo.

Aidha shabiki yeyote atakayekiuka maagizo hayo atakumbana na adhabu ya kufukuzwa uwanjani, kuripotiwa katika jeshi la polisi na ikiwa atafanya zaidi ya mara moja anaweza kufungiwa kabisa kuhudhuria michuano hiyo.

Licha ya mashabiki kupigwa marufuku kuvuta sigara na bangi viwanjani lakini sheria mpya nchini humo imeruhusu utumiaji wa bangi hadharani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post