Martinez kurudi tena uwanjani

Martinez kurudi tena uwanjani

Mchezaji wa #ManchesterUnited, #LisandroMartinez anatarajiwa kurudi tena uwanjani katika mchezo wa fainali ya kombe la FA utakaochezwa Mei 25, 2024 katika uwanja wa #Wembley nchini Ungereza.

Martinez mpaka kufikia sasa amekosa ‘mechi’ 37 kati ya 48 za ‘klabu’ hiyo msimu huu kwenye michuano yote kutokana na majeraha ya mguu, hali iliyopelekea matokeo yasiyoridhisha ikiwemo kipigo cha 4-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumatatu.

Man United ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ‘Ligi’ kuu #England inaelekea kushindwa kushiriki michuano ya Ulaya huku kombe la FA likitazamiwa kuwa njia pekee ya kuiwezesha kushiriki walau kwenye’ligi’ ya Europa ikiwa watapata ushindi mbele ya Mabingwa watetezi, Manchester City.

Beki huyo mwenye umri wa mika 26, raia wa Argentina alingia ‘klabuni’ hapo July mwaka 2022 akitokea ‘timu’ ya #Ajax.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post