Mark ajishusha kwa familia zilizoumizwa na mitandao

Mark ajishusha kwa familia zilizoumizwa na mitandao

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya #Meta, #MarkZuckerberg ameomba radhi kwa familia zinazodai watoto wao waliathiriwa na maudhui ya mitandao ya kijamii.

Zuckerberg ambaye anamiliki #WhatsApp #Instagram na #Facebook amesema hayo katika mkutano wa Bunge nchini Marekani ambapo ulihusisha viongozi wa Tiktok, #Snapchat, X(Twitter) na Discord.

Hata hivyo Wabunge walitaka kujua hatua zinazochukuliwa kuwalinda watoto mitandaoni, ambapo pia walizungumza na baadhi ya familia ambazo zilisema watoto wao walijidhuru na wengine kujiua kutokana na maudhui ya mitandao ya kijamii.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags