Marioo na Mr Nice wana jambo lao

Marioo na Mr Nice wana jambo lao

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Mr Nice ameamua kurudi mjini kivingine baada ya kutangaza ujio wa wimbo mpya ambao ameshirikishwa na Marioo walioupa jina la ‘Shisha’.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mr Nice ametoa ya moyoni kwa kueleza kuwa ni heshima kubwa kutoka kwa  Marioo baada ya kumtafuta na kutaka wafanye kazi pamoja. Mr Nice amdai kuwa anaamini wimbo huo utafanya vizuri na utakuwa wa kufungia mwaka.

Mr Nice alitamba na vibao kama ‘Fagilia’, ‘Kikulacho’, ‘Mbona umeniacha’ na ile ya ‘Kila Mtu na Demu wake’ huku wimbo wake wa mwisho kuuachia katika mtandao wake wa YouTube ukiwa ni ‘I Swear’ uliotoka miezi sita iliyopita.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags