Marehemu aliyehifadhiwa kwa miaka 128 kuzikwa week hii

Marehemu aliyehifadhiwa kwa miaka 128 kuzikwa week hii

Yamekuwa yakitokea matukio kwa baadhi ya miili ya watu kuchelewa kuzikwa baada ya kufariki kutokana na sababu mbalimbali kama vile za kifamilia, uchunguzi na nyinginezo.

Mwaka huu umeingia kwenye historia kutokana na mwili wa mwanaume aliyefariki Novemba 19, 1895, kuzikwa week hii baada ya maiti yake kukaa bila kuzikwa kwa takribani miaka 128.


mwanaume huyo alipewa jina la Stoneman Willie alifariki akiwa Gerezani baada ya kukamatwa kwa wizi, alifariki miaka 128 iliyopita baada ya figo yake kushindwa kufanya kazi kutokana kwa madai ya kuwa mlevi kupindukia kipindi cha uhai wake.

Licha ya kupewa jina la Stoneman Willie, mwanaume huyo baada ya kufariki alikosa ndugu wa kumzika kutokana kutotambuliwa kwani baada ya kukamatwa alidanganya jina na inadaiwa hakutumia jina lake halisi.

Mwili Stoneman baada ya kufariki uliwekwa kwenye jumba la huduma ya mazishi huko Reading, Pennsylvania.

Hivyo kulingana na mwanahistoria wa eneo hilo George M. Meiser XI, mwili huo ulihifadhiwa na , mtaalamu wa maiti Theodor Auman, kwa lengo la kuufanyia majaribio ya njia ya kuhifadhi maiti kwa muda mrefu.

Kwani wakati huo maiti zilikuwa zikihifadhiwa kwenye barafu kwa hiyo mbinu mpya ya uhifadhi maiti ilifanyiwa majaribio kwa mwanaume huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags