Mapya yaibuka kesi ya Diddy

Mapya yaibuka kesi ya Diddy

Wakati msako wa kumsaka ‘rapa’ Diddy ukiendele nchini Marekani mapya yaibuka ambapo imeripotiwa kuwa ‘rapa’ Yung Miami alihusika  kumbebea Diddy dawa za kulevya aina ya ‘Pink Cocaine’.

Kwa mujibu wa nyaraka za kesi iliyofunguliwa na mtayarishaji Rodney Jones dhidi ya Diddy imedai kuwa dawa hizo za kulevya zilizobebwa na Yung zilisafirishwa na ndege binafsi ya Diddy ambapo zilitoka Miami hadi Virginia sehemu ambayo Diddy alikuwepo akifanya ‘Reheso’ kwa ajili ya tamasha lake la ‘Something In The Water’ la mwaka 2023.

Dawa hizo zilipelekwa huko baada ya Diddy kuonekana hayuko sawa ambapo mbeba madawa wa kulevya wa Diddy alisahau kubeba ndipo akamtuma ‘rapa’ Yung kusafirisha mzigo huo.

Ikumbukwe kuwa Rodney Jones ni moja ya mhanga aliyefungua kesi ya unyanyazaji wa kingono dhidi ya Diddy ambapo katika maelezo yake alidai kuwa alifanyiwa ukatili wa kulazimishwa kufanya ngono na wanawake wanaojiuza, kudhulumiwa malipo ya uandaaji wa 'The Love Album: Off the Grid' iliyotoka mwaka jana na madai mengine.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags