Maporomoko ya ardhi kaskazini mwa Venezuela yamesababisha vifo vya takriban watu watatu, huku uharibifu mkubwa ukiripotiwa huko el Castano, wilaya ya Maracay, mji mkuu wa jimbo la Aragua, ulioko kilomita 83 kutoka mji mkuu Caracas.
Picha za televisheni nchini Venezuela zilionyesha maporomoko ya ardhi yakisomba magari, miti na mawe makubwa pamoja na makazi ya watu.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametoa taarifa hiyo wakati wa hotuba yake huko Las Tejerías, ambapo maporomoko ya ardhi yalisababisha vifo vya watu 54 na wanane kutoweka wiki moja iliyopita.
Chanzo DW
Leave a Reply