Manula atemwa Simba, watambulishwa wanne

Manula atemwa Simba, watambulishwa wanne

Aliyekuwa kipa namba moja wa Simba, Ashi Manula ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo msimu 2024/25 baada ya timu hiyo kutambulisha makipa wanne huku jina lake likiondolewa.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ndiye alikuwa anatambulisha mastaa wa kikosi hicho msimu ujao alitaja majina manne eneo la kulinda mlango ambao ni Ally Salim, Ayoub Lakred, Mohammed Camara na Hussein Abel ndio idadi ya makipa ambao wataiongoza Simba eneo la goli kipa.

Wakati wa kutaja majina hayo nyomi ya mashabiki iliyojaza uwanja wa Mkapa iliibua shangwe baada ya kusikia jina la Lakred ambaye inaelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na kuumia akiwa mazoezini huko Misri.

Pia shangwe kubwa imeibuka baada ya kutajwa kwa kipa mpya wa timu hiyo ambaye amesajiliwa kwa lengo la kuziba pengo la Lakred ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha alilolipata.

“Hawa ndio walinda mlango ambao tutakuwa nao msimu ujao.” Amesema Ahmed.

Imeandikwa na Charity James






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags