Mandonga: Simfahamu Mwakinyo

Mandonga: Simfahamu Mwakinyo

Bondia kutoka nchini Tanzania Karim Mandonga, kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari amedai kuwa hamfahamu bondia Hassan Mwakinyo.

Mandonga amesema hayo baada ya kuambiwa kuhusiana na kauli ya Mwakinyo aliyodai kuwa yupo tayari kupigana bondia yeyote nchini kwa laki tano kila 'raundi' moja.

Katika majibu yake alisema

“Hassan mwakinyo ni nani huyo, bondia kama huyo sijawahi kumsikia kwa Tanzania nawajua mabondia wengi sana lakini jina hilo ulilo nambia, Mwakinyo kwa Tanzania hatuna bondia wa hivyo Tanzania nzima.

Nawafahamu mabondia wengi wakina, Twaha Kiduku, Seleman Kidunda, Mfaume Mfaume, na wengine lakini bondia huyo simfahamu”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags