Mandonga mtu kazi aja kivingine

Mandonga mtu kazi aja kivingine

Weeeuuweeee! I hope mko good watu wangu wa nguvu na natumai wote mmehesabiwa eeeh, habari nzuri bwana ni kutoka  kwa mtu kazi baada ya kuonesha uwezo alionao licha ya kuwa na baadhi ya watu kumdharau kuwa hawezi ngumi.

Bondia Karim Mandonga ameibuka kidedea katika pambano la uzito wa kati baada ya kumpiga Bondia Sotii Mdudu kutoka Kigoma kwa Technical Knockout (TKO) katika round ya 4 ambapo mpambano huo ulikuwa ni wa round 8.

Aidha pambano hilo limechezwa Kigoma katika fukwe za ziwa Tanganyika Kidyama ambapo Mashabiki wa Mchezo huo Kigoma walishuhudiwa wakijitokeza kwa wingi kutazama pambano hilo.

baada ya mpambano huo kupitia ukurasa wake wa instagram bondia huyo aliandika kuwa " hii ndo maana halisi ya kumpiga mtu kama ngoma wajipange" ameandika Karim Mandonga






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags