Mandonga afungiwa kushiriki ngumi

Mandonga afungiwa kushiriki ngumi

Baada ya bondia #KareemMandonga kuingia ulingoni mfululizo bila kupata mapumziko ambayo yataweza kumuweka ‘fiti’ kwaajili ya mapambano mengine, bondia huyo hatoshiriki tena ngumi mpaka atakapopimwa afya yake.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) ikieleza kuwa bondia huyo wa ngumi za kulipwa hatoshiriki mapambano ya ngumi mpaka atakapo pimwa Afya hii ni baada ya kipigo cha TKO katika pambano lake na #MasesGolola kutoka #Uganda lilifanyika julai 92 mwaka huu huko Mwanza

Akizungumza na Swahili Times, Katibu wa TPBRC, #GeorgeLukindo amesema Mandonga anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi Agosti 15 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majibu ya uchunguzi ndiyo yatatoa majibu endapo ataruhusiwa kucheza pambano lake litakalofanyika Agosti 27 mwaka huu visiwani #Zanzibar.

“Kwa kawaida anafungiwa kwanza, mazoezi anaweza kufanya kwa sababu ni afya siyo yeye tu ila kwa sababu Mandonga ni maarufu Tanzania lakini bondia wote wanafanyiwa hivyo hivyo, anafungiwa ndani ya mwezi mmoja anafanyiwa matibabu, baada ya daktari mwenyewe kujiridhisha anaweza akaeleza kama anaweza kuendelea na pambano kama kawaida au la,” amesema.

Mandonga atakuwa ndani ya kifungo mpaka Septemba 13 mwaka huu na mpaka sasa hakuna dalili yoyote mbaya ambayo ameionesha ya kuwa kunashida kwenye Afya yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags